UWASE · LEGAL FRAMEWORK

UWASE Constitution

The official Constitution of the Association of Wanyaseka Living Outside Seka (UWASE), effective 1 January 2026.

Dibaji Sura ya 1: Jina na Madhumuni Sura ya 2: Uanachama Sura ya 3: Uongozi Sura ya 4: Mikutano Sura ya 5: Fedha na Ada Sura ya 6: Ustawi na Misaada Sura ya 7: Marekebisho

Dibaji (Preamble)

Sisi, Wanyaseka tunaoishi nje ya Kijiji cha Seka, tukitambua umuhimu wa kuunganisha nguvu, kusaidiana katika shida na faraja, na kuchangia maendeleo endelevu ya Kijiji chetu cha Seka na jamii yetu yote, kwa pamoja tumekubaliana kuunda umoja huu unaoitwa UWASE.

Sura ya 1: Jina, Makao Makuu na Madhumuni

1.1 Jina: Jina la umoja huu ni Umoja wa Wanyaseka Wanaoishi Nje ya Seka (kwa kifupi: UWASE).

1.2 Makao Makuu: Makao makuu ya Umoja yapo Kijiji cha Seka, Mkoa wa Mara. Anuani rasmi ya posta ni S.L.P 717, Musoma Mara.

1.3 Misingi Mikuu: Umoja umejengwa katika misingi ya Uhuru, Undugu, Amani, Usawa na Demokrasia.

1.4 Madhumuni ya Umoja:

  • Kuongeza mshikamano na undugu miongoni mwa Wanyaseka bila ubaguzi wa rangi, jinsia, dini au kabila.
  • Kushirikiana, kusaidiana na kufarijiana katika hali zote za shida na faraja.
  • Kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo kwa wanaumoja na familia zao.
  • Kujitolea na kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kijiji cha Seka.
  • Kuwa mfano bora wa kuigwa wa ushirikiano na uadilifu katika jamii.

Sura ya 2: Uanachama, Sifa, Haki na Wajibu

2.1 Sifa za Mwanachama: Mwanachama anapaswa kuwa Mtanzania mwenye umri wa miaka 25 au zaidi, anayejitegemea kiuchumi, mwenye nidhamu na tabia njema, ambaye maombi yake yameidhinishwa na Kamati Tendaji na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu.

2.2 Ada ya Kiingilio na Michango: Kila mwanachama anapaswa kulipa ada ya kiingilio ya TZS 100,000 na ada ya mwezi ya TZS 10,000 (au TZS 120,000 kwa mwaka).

2.3 Wategemezi: Mwanachama ana haki ya kusajili mwenza (mume/mke), watoto sita (6), na wazazi wawili (baba na mama mzazi).

Sura ya 3: Muundo wa Uongozi

Uongozi wa UWASE unajumuisha Bodi ya Wadhamini na Kamati Tendaji inayoundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mhazini Msaidizi, Mkaguzi wa Hesabu na Wajumbe wanne.

Sura ya 5: Fedha, Ukaguzi na Usimamizi

Mali na fedha zote za UWASE zitawekwa kwenye akaunti rasmi ya benki. Miamala yote inahitaji saini zilizoidhinishwa za viongozi wakuu. Hesabu za Umoja zitakaguliwa kila mwaka na Mkaguzi wa Hesabu na taarifa kusomwa kwenye Mkutano Mkuu.

Download Complete Constitution

Download or request the official print copy from the executive secretariat.

Go to Downloads