UWASE · MWONGOZO WA UANACHAMA

Uanachama na Kujiunga na UWASE

UWASE inakaribisha Wanyaseka wote wanaoishi nje ya Seka na waliopo Seka kujiunga ili kujenga umoja imara, kusaidiana na kuinua Kijiji chetu.

1

Jaza Maombi

Wasiliana na Katibu au jaza fomu rasmi ya maombi ya uanachama.

2

Uhakiki wa Kamati

Kamati Tendaji itakagua na kuhakiki taarifa zako kwa mujibu wa Katiba.

3

Lipa Kiingilio

Lipa ada ya kiingilio ya TZS 100,000 kupitia akaunti rasmi ya benki.

4

Kadi na Katiba

Pokea namba ya uanachama, nakala ya Katiba na sajili familia yako.

Ada na Michango ya Kifedha

Aina ya AdaKiasi (TZS)MzungukoMaelezo
Ada ya KiingilioTZS 100,000Mara MojaInalipwa wakati wa kukamilisha usajili mpya
Ada ya Kila MweziTZS 10,000Kila MweziAda ya uendeshaji wa Umoja na mifuko ya ustawi
Ada ya Mwaka MzimaTZS 120,000Kila MwakaMwanachama anaweza kulipa jumla kwa mwaka mzima

Usajili wa Familia na Wategemezi

Rejista ya UWASE inajumuisha:

  • Mwanachama Mwenyewe
  • Mwenza wa Ndoa
  • Watoto hadi sita (6)
  • Wazazi wawili (Baba na Mama mzazi)

Je, uko tayari kujiunga na UWASE?

Wasiliana na Katibu au tuma ujumbe sasa kupitia fomu ya mawasiliano.

Wasiliana Nasi / Tuma Maombi