Uanachama na Kujiunga na UWASE
UWASE inakaribisha Wanyaseka wote wanaoishi nje ya Seka na waliopo Seka kujiunga ili kujenga umoja imara, kusaidiana na kuinua Kijiji chetu.
1
Jaza Maombi
Wasiliana na Katibu au jaza fomu rasmi ya maombi ya uanachama.
2
Uhakiki wa Kamati
Kamati Tendaji itakagua na kuhakiki taarifa zako kwa mujibu wa Katiba.
3
Lipa Kiingilio
Lipa ada ya kiingilio ya TZS 100,000 kupitia akaunti rasmi ya benki.
4
Kadi na Katiba
Pokea namba ya uanachama, nakala ya Katiba na sajili familia yako.
Ada na Michango ya Kifedha
| Aina ya Ada | Kiasi (TZS) | Mzunguko | Maelezo |
|---|---|---|---|
| Ada ya Kiingilio | TZS 100,000 | Mara Moja | Inalipwa wakati wa kukamilisha usajili mpya |
| Ada ya Kila Mwezi | TZS 10,000 | Kila Mwezi | Ada ya uendeshaji wa Umoja na mifuko ya ustawi |
| Ada ya Mwaka Mzima | TZS 120,000 | Kila Mwaka | Mwanachama anaweza kulipa jumla kwa mwaka mzima |
Usajili wa Familia na Wategemezi
Rejista ya UWASE inajumuisha:
- Mwanachama Mwenyewe
- Mwenza wa Ndoa
- Watoto hadi sita (6)
- Wazazi wawili (Baba na Mama mzazi)